/*URL: http://www.AllBlogTools.com/ */ .basictab{ padding: 3px 0; margin-left: 0; font: bold 12px Verdana; border-bottom: 1px solid gray; list-style-type: none; text-align: left; /*set to left, center, or right to align the menu as desired*/ } .basictab li{ display: inline; margin: 0; } .basictab li a{ text-decoration: none; padding: 3px 7px; margin-right: 3px; border: 1px solid gray; border-bottom: none; background-color: #f6ffd5; color: #2d2b2b; } .basictab li a:visited{ color: #2d2b2b; } .basictab li a:hover{ background-color: #DBFF6C; color: black; } .basictab li a:active{ color: black; } .basictab li.selected a{ /*selected tab effect*/ position: relative; top: 1px; padding-top: 4px; background-color: #DBFF6C; color: black; }

Saturday, April 4, 2015

EDDIE MURPHY

                MJUE EDDIE MURPHY KWA UFUPI






 Jina lake kamili ni Edward Regan Murphy.
Amezaliwa mnamo April 3, 1961 Brooklyn, New York Marekani.



                                      KAZI YAKE

Ni mwigizaji, Mchekeshaji, Mwimbaji na ni Muandaaji wa filamu



                                      MAISHA YAKE KWA UFUPI

Akiwa ni mtoto wa Lilian na Charles Edward Murphy, Eddie alivutiwa na tasnia ya sanaa ya Vichekesho tangu utotoni mwake huku akivutiwa sana na mchekeshaji Bill Cosby. Jina lake lilianza kuwa maarufu baada ya kufanya vizuri kwenye show ya Saturday Night Live miaka ya 1980's



                                      FILAMU ALIZOSHIRIKI

Tower Heist - 2011 (Slide)
Imagine That - 2009 (Evan Danielson)
I Spy - 2002 (Kelly)
Holy Man - 1998 (G)
Norbit - 2007 (Muandaaji)

Ameshiriki pia mfululizo wa filamu ya SHREK  kama sauti ya Donkey kati ya 2001 - 2010.. Ameshirika filamu nyingine nyingi pamoja na show za Televisheni kama Father of the Pride (2004), The PJs  nk.



                                    TUZO

Golden Globes (2007) - Filamu DreamGirls (2006)
AAFCA (2006) -  Filamu DreamGirls (2006)
Annie Awards (2001) - Filamu Shrek (2001)
Image Awards (1983) - Trading places (1983)

Pia ametajwa (Nominated) na kushinda tuzo nyingine nyingi.



                                   TRIVIA

Eddie amefanya ameshirikiana (Collaborated) na Msanii Shaba Ranks kwenye wimbo uitwao  ''I was a King'', Ameimba wimbo ''Red Light'' akimshirikisha Snoop Lion, Moja kati ya nyimbo za kukumbukwa za Eddie Murphy ni ''How could it Be''.

Sunday, July 21, 2013

BI KIDUDE

MJUE BI KIDUDE KWA UFUPI



Jina lake kamili ni Fatuma Binti Baraka,amezaliwa mnamo miaka ya 1910's huko Zanzibar.

Amefariki mnamo Tarehe 17 April 2013.

KAZI YAKE
Mwimbaji wa muziki aina ya Taarab pia ni kungwi.

MAISHA YAKE KWA UFUPI

Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo huko Tanzania visiwani/Zanzibar,alikuwa ni binti wa mfanya biashara ya nazi..Bi kadude alilazimika kukimbilia Dar es salaam baada ya kulazimishwa aolewe akiwa na umri wa miaka 13.
Rekodi zake kimuziki zilianza miaka ya 1930's.
Miaka ya 1940's alirudi tena Zanzibar na kuendelea na shughuli zake.
Miongoni mwa nyimbo alizofanya ni pamoja na YA LAITI M,UHOGO WA JANGOMBE,KIJITI,BOMWAZANI WA MAHABA,BERU NK. Pia ameshirikishwa kwenye nyimbo kadhaa kama Ahmada ya Offside Trick,Juhudi za wasiojiweza na Fid Q nk.

TUZO

* WOMEN AWARD 2005
* Sports and Arts award of all time 2012 ambayo alitunukiwa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

TRIVIA

Inasadikika Bi Kidude hakufanikiwa kuwa na mtoto wa kuzaa.

BAADHI YA VIDEOS







Wednesday, April 24, 2013

AZRA AK


MJUE AZRA AK KWA UFUPI






Jina lake kamili ni Azra Ak amezaliwa 8 December 1981 huko Almelda,Netherland.



KAZI YAKE
Ni mwanamitindo mwigizaji na ni mshindi wa Shindano la Miss World mwaka 2002 lililofanyika huko Alexander palace UK,


MAISHA YAKE KWA UFUPI

Azra amezaliwa na wazazi wenye asili ya kituruki,Amewahi pia kuwa miss uturuki mwaka 2002.
Amewahi kushiriki mashindano mbalimbali huko  Ufaransa,Uturuki na Ujerumani.


TUZO

*Medali ya dhahabu mshindi wa British TV Reality show iitwayo THE GAME 2003
*Mshindi wa show ya mashindano ya kucheza ya YOK BOYLE DANS 2010

FILAMU ALIZOWAHI KUSHIRIKI

*Anlat Istanbul - 2004
*Teberik Sanss - 2005
*Ik Ask Bahar - 2006
*PesPesse - 2010

Pia ameshiriki show mbalimbali za TV kama vile

*The Game 2003
*Ya mur zaman 2004
*National songfestival 2009
*Muck 2012
............

TRIVIA

Azra ana kimo cha futi 5 na inchi 7 [1.7m]
Ana macho ya brown na nywele nyeusi

Tuesday, January 22, 2013

BALLY SAGOO

MJUE BALLY SAGOO KWA UFUPI



Jina lake kamili ni Baljit Singh Sagoo
Amezaliwa 19 May 1971 huko Delhi India

KAZI YAKE

Ni mwimbaji mahadhi ya Bhangra,Fusion na Pop.Pia ni DJ,Mwandishi wa mashairi na Mtayarishaji wa Muziki.


MAISHA YAKE KWA UFUPI

Bally Sagoo ni mzaliwa wa India ila amekulia na kuishi huko Birmigham England.Ameanza muziki mnamo mwaka 1989 na ni miongoni mwa waasisa wa uimbaji mahadhi ya Bhangra Fusion hivyo pia anafahamika kama 'The Godfather of Bhangra'.


Bally amefanikiwa kuanzisha lebo yake mwenyewe inayoitwa ISHQ RECORD Mnamo mwaka 1998.
Sagoo amewahi kupata tuzo ya Mwimbaji anayefanikiwa katika ''UK ASIAN MUSIC AWARD'' Mwaka2003.

ALBAMU

Bally amefanya albam nyingi hizi ni chache kati ya hizo

*Rising from East 1996
*Hanji 2003
*Dub of Asia 2001
*Play the game 2006
*Bollywood flashback 1994
*Star crazy 2 2007
*The best of Bally Sagoo 2007
*Aaja Nachle 1998
*Ragga Muffin 1991
...............



TRIVIA

Inasemwa kuwa Bally Sagoo amesitisha kuimba na kujikit zaidi kwenye utayarishaji wa muziki na uandishi wa mashairi mnamo mwaka 2009

BAADHI YA NGOMA ZAKE

AAJA NACHLE 



BILO NI TERA


PUNJABIYAN DI HOGI

Sunday, January 13, 2013

HIFIKEPUNYE POHAMBA

MJUE HIFIKEPUNYE POHAMBA KWA UFUPI



Jina lake kamili ni Hifikepunye Lucas Pohamba,Mzaliwa wa Okanghundi huko Namibia.
Amezaliwa Agosti 18,1935

KAZI YAKE

Ni Raisi wa pili wa Jamhuri ya Namibia kupitia chama cha SOUTH WEST PEOPLE'S ORGANIZATION [SWAPO] baada ya Sam Nujoma 1990-2005.Ni raisi wa sasa mpaka kufikia uchaguzi wa 2014.

MAISHA KWA UFUPI

Mkewe anaitwa Penehufipo Pohamba,ni baba wa watoto watatu,Kaupu,Tulongeni na Ndapandula.
Pohamba amekulia katika maisha ya kiroho ya dhehrbu la Anglican ambapo pia alipata elimu yake katika shule ya kimishenari...Kufikia umri wa miaka 25 Pohamba alijikita kwenye siasa ndani ya chama cha South West People's Organization[SWAPO].
Aliwahi kuwa mfungwa wa kisiasa ambapo alitumikia miezi minne jela na baadae kifungucha ndani miaka miwili.

NYADHIFA KABLA HAJAWA RAISI

*Waziri wa mambo ya ndani 1990-1995
*Waziri wa uvuvi na rasirimali za majini 1995-1997
*Waziri asiya na wizara maalum 1997-2000
*Katibu mkuu wa SWAPO 1997
*Makamu m/kiti wa SWAPO 2002
*Waziri wa ardhi 2001-2005

Pohamba alishinda katika uchaguzi wa 2009.

TRIVIA

*Alipata takribani kura 213 kati ya 526 katika raundi ya kwanza ya uchaguzi wa 2004 na kura 341 katika raundi ya pili.
*Amewahi kupata tuzo ya ujasiri ''Ongulumbashe Medal''
...........................  

Monday, January 7, 2013

JOHN R. LEONETTI

MJUE JOHN LEONETT KWA UFUPI


Jina lake kamili ni John Robert Leonetti.
Amezaliwa Julai 4,1956 huko California Marekani.

KAZI YAKE

Ni mchukuaji wa picha/video za filamu ''Cinematographer'' Pia ni Muongozaji wa filamu ''Direcctor''
Alianza rasmi kujikita kwenye masuala ya filamu mnamo mwaka 1991.Amekuwa kama directer  kwenye filamu 1(Insidious),Kama mchukua picha kwenye filamu 33,Kama director kwenye filamu 4.

FILAMU ALIZOFANYIA KAZI KAMA CINEMATOGRAPHER

*Dead silence 2007
*Death sentence 2007
*Piranha 3D 2010
*Soul surfer 2011
*Child's play 3 1991
*The scorpion king 2002
*The Mask 1994
*Spy hard 1996
*..............

Pia The Butterfly Effect na Mortal Kombat Annihilation kama Director pamoja na Mortal Kombat part 1 kama director of photography.

TRIVIA

*Leonetti ni ndugu wa mtayarishaji mwingine aitwaye  Mathew F. leonetti
*Mwanachama wa American Society of Cinematographers ASC tangia 2003
...................

Monday, December 31, 2012

THE CELEB'S PROFILE

                   MJUE ''RONALDINHO GAUCHO KWA UFUPI


Jina lake kamili ni Ronaldo de Assin Moreira.
Ana urefu wa 1.81cm.
Amezaliwa tarehe 21 Machi 1980 huko Porto Alegre-Rio Grande do sul Brazil.
Ni mchezaji wa mpira wa miguu nafasi ya kiungo mshambuliji{Midfielder/Forward}.

KLABU ALIZOCHEZA
Gremio 1998-2001
Paris saint Germain 2001-2003
Barcelona 2003-2008
Milan 2008-2010
Flamengo 2011-2012
Atletico Mineiro 2012-


MAISHA KWA UFUPI

Ndoto yake ya kuwa mchezaji ilianza akiwa na umri wa miaka 8 na ndicho kipindi alichopewa jina la Ronaldinho kutokana na alikuwandiye mchezaji mdogo na mfupi zaidi kwenye klabu aliyochezea.
Alianza kufahamika mwaka 1997 kwenye ubingwa wa dunia chini ya umri wa miaka 17 huko nchini Misrialipofunga mabao mawili kwa mikwaju ya penati.

Ronaldinho ana mtoto mmoja aitwaye JOAO aliyezaa na Janaina Mendez mnamo Februari 25 mwaka 2005.

TUZO

Mchazaji Bora wa mwaka wa FIFA mwaka 2004 na 2005 pia mchezaji bora wa ulaya......continues

TRIVIA

*Ni mchezaji wa kibrazil mwenye soko zaidi duniani
*Amefanya matangazo na kampuni kubwa zaidi kama PEPSI,NIKE,LENOVO nk