Jina lake kamili ni Hifikepunye Lucas Pohamba,Mzaliwa wa Okanghundi huko Namibia.
Amezaliwa Agosti 18,1935
KAZI YAKE
Ni Raisi wa pili wa Jamhuri ya Namibia kupitia chama cha SOUTH WEST PEOPLE'S ORGANIZATION [SWAPO] baada ya Sam Nujoma 1990-2005.Ni raisi wa sasa mpaka kufikia uchaguzi wa 2014.
MAISHA KWA UFUPI
Mkewe anaitwa Penehufipo Pohamba,ni baba wa watoto watatu,Kaupu,Tulongeni na Ndapandula.
Pohamba amekulia katika maisha ya kiroho ya dhehrbu la Anglican ambapo pia alipata elimu yake katika shule ya kimishenari...Kufikia umri wa miaka 25 Pohamba alijikita kwenye siasa ndani ya chama cha South West People's Organization[SWAPO].
Aliwahi kuwa mfungwa wa kisiasa ambapo alitumikia miezi minne jela na baadae kifungucha ndani miaka miwili.
NYADHIFA KABLA HAJAWA RAISI
*Waziri wa mambo ya ndani 1990-1995
*Waziri wa uvuvi na rasirimali za majini 1995-1997
*Waziri asiya na wizara maalum 1997-2000
*Katibu mkuu wa SWAPO 1997
*Makamu m/kiti wa SWAPO 2002
*Waziri wa ardhi 2001-2005
Pohamba alishinda katika uchaguzi wa 2009.
TRIVIA
*Alipata takribani kura 213 kati ya 526 katika raundi ya kwanza ya uchaguzi wa 2004 na kura 341 katika raundi ya pili.
*Amewahi kupata tuzo ya ujasiri ''Ongulumbashe Medal''
...........................
No comments:
Post a Comment